Back to Search Start Over

Ulinganishi wa Ngeli za Nomino za Lugha za 'Runyačitara'1

Authors :
Asiimwe, Caroline
Source :
Kiswahili; Vol 18, No 1 (2018); 78-95
Publication Year :
2019
Publisher :
University of Dar es Salaam, 2019.

Abstract

“Runyačitara” ni lugha zinazozungumzwa Magharibi mwa Uganda na zina uhusiano unaofanya baadhi ya wanazuoni kuhisi kwamba ni lahaja za lugha moja. Makala hii inahusika na ulinganishi wa ngeli za nomino za lugha zote nne za “Runyačitara”. Ulinganishi wa ngeli za nomino katika lugha hizi umefanywa kwa kuegemea namna maneno yanavyojitokeza kwa kuzingatia viambishi, maana na dhima za viambishi hivyo katika lugha hizi. Makala inafafanua kwamba uainishaji wa ngeli za nomino unaweza kufanywa kwa kuegemea mikabala tofautitofauti kulingana na wanazuoni tofauti. Hata hivyo, ulinganishi wa lugha za Runyačitara kwa kuegemea mikabala hiyo umeonesha kwamba lugha hizi zina mfanano wa hali ya juu - hali inayoonesha kwamba zina uhusiano wa karibu.

Details

Language :
English
ISSN :
00231886
Database :
OpenAIRE
Journal :
Kiswahili
Accession number :
edsair.78975075580c..c208568a3ecef6cbb0caeae322935f6d